tmoja2

Video: Yanga yailaza Ndanda 4-0. Tazama magoli yote yaliyofungwa hapa

303
0
Share:
Share this
tmoja2

Klabu ya Yanga leo imeshuka dimbani kucheza dhidi ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara ambapo Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli manne na kujihakikishia alama tatu muhimu.

Kufuatia ushindi wa leo, Yanga wamefikisha jumla ya alama 40 wakiwa wamecheza michezo 18 na kushika nafasi ya pili, ikiwa ni alama moja nyuma Simba wenye alama 41 baada ya kucheza michezo 17 wakiongoza ligi.

Wafungaji wa magoli ya Yanga leo ni Donald Ngoma aliyefunga magoli mawili, Amiss Tambwe na Vicent Bossou ambao wote wamefunga goli moja kila mmoja.

Hapa chini ni video za magoli yote ya Yanga.

Goli la kwanza lililofungwa na Donald Ngoma dakika ya 4.

Goli la pili la Yanga lililofungwa tena na Donald Ngoma

Amiss Tambwe akiifungia Yanga goli la tatu

Goli la nne la Yanga lililofungwa na Vicent Bossou

Comments

error: Content is protected !!