tmoja2

Vikao vya majadiliano ya kutafuta suluhu ya kudumu baina ya kambi ya upinzani na Naibu Spika kuanza.

3905
0
Share:
Share this
Kambi rasmi ya upinzani imepanga kufanya vikao vya kujadili suluhu ya kudumu ya mgogoro na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson uliosababisha wabunge wanaounda Ukawa kususia vikao vinavyoendeshwa na kiongozi huyo.
Vikao hivyo vinapangwa kufanyika wakati mkutano wa nne ukianza rasmi kesho, baada ya kuahirishwa wakati wa mkutano wa Bajeti mwishoni mwa Juni mwaka huu .
Mbunge wa Vunjo (NCCR- Mageuzi), James Mbatia ambaye ni msemaji wa Upinzani Bungeni alieleza kuwa uamuzi wa kufanya vikao hivyo umefikiwa baada ya upinzani kukaa kikao na viongozi wa dini Agosti 24 mwaka huu ili kutafuta suluhu ya kudumu na kisha, kutangaza kurudi bungeni baada ya mkutano wao na viongozi wa dini.
Wabunge wa Upinzania walikuwa wakisusia vikao vilivyokuwa vikiendeshwa na Naibu Spika kwa madai ya kutoridhishwa na uongozi wake tangu Mei mwaka huu, baada ya Dk Tulia kukataa kujadili hoja ya kufukuzwa wanafunzi zaidi ya 8,000 stashahada ya ualimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

Comments

error: Content is protected !!