tmoja2

Wabunge wanawake wa UKAWA watoka bungeni

122
0
Share:
Share this
tmoja2

Mbunge wa Kawe Halima Mdee na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) amealani kitendo cha Mbunge wa CCM kuwadhihaki Wabunge wa viti maalum wa UKAWA hususani CHADEMA.

” Mdee ameeleza kwa, wakati Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) akichangia hotuba ya Wizara ya Katiba na Sheria alisema wabunge wa UKAWA hususani CHADEMA hawawezi kupata ubunge wa viti maalumu hadi pale wanapokuwa na mahusiasno ya kimapenzi na viongozi wa chama”.

Mdee amesema kuwa kauli hiyo imewadhalilisha sana kwani analolisema Mlinga sio kweli hata kidogo kwani wao kama chama wanataratibu zao za kupata wabunge wa viti maalumu.

Aidha kilichowakwaza zaidi ni kitendo cha Naibu Spika ambaye pia ni mwanamke kulichukulia jambo hilo kiwepesi sana. Kingine ni suala la baadhi ya wabunge wa CCM kushangilia, ni dhahiri wamedhalilishwa hivyo wabunge wanawake wa UKAWA wametangaza kujiondoa kwenye umoja wa wabunge wanawake na kuwaacha wanawake wabunge wa CCM pekee.

Comments

error: Content is protected !!