tmoja2

Wachezaji na mashabiki wafariki dunia baada ya boti kuzama Ziwa Albert, Uganda

198
0
Share:
Share this
tmoja2

Takribani watu 30 wanahofiwa kuwa wamekufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Albert nchini Uganda mapema leo.

Boti hiyo ilikuwa imebeba wachezaji na mashabiki waliokuwa wanakwenda kwenye mchezo wa mpira wa miguu maaluum kwa ajili ya Krismasi katika Wilaya ya Hoima wakitokea Buliisa.

Taarifa za Polisi zinaeleza kuwa boti hiyo ilikuwa na watu 45 na ilizama baada ya abiria wote kuegemea upande mmoja wa boti. Idadi hiyo kubwa ya abiri imezidi uwezo wa boti hiyo kubeba.

Taarifa zinazsema kuwa miili ya watu 9 imepatikana huku wengine 15 wakiokolewa huku wengine 21 wakiwa hawajulikani walipo.

Ajali za kuzama kwa boti katika ziwa Albert zimekuwa zikitokea mara kwa mara ambapo chanzo kikubwa kinadaiwa ni ubovu a boti pamoja na kuzidisha abiria.

Mwezi wa 11 watu wengine 11 walifariki baada ya kuzama katika Ziwa Albert.

Comments

error: Content is protected !!