tmoja2

Watu 30 wakamatwa, watumishi wawili wasimamishwa kazi kufuatia mauaji mkoani Dodoma

2980
0
Share:
Share this
tmoja2

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikiliwa watu 30 kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watafiti watatu wa Kituo cha Utafiti wa Udongo na Maendeleo ya Ardhi cha Selian mkoani Arusha.

Hayo yamesema leo katika kijiji cha Iringa Mvumi na Kamanda wa Polisi mkoa Dodoma Lazaro Mambosasa. Kamanda Lazaro alifafanua kuwa wanaoshikiliwa hadi sasa ni wanawake tisa na wanaume 21 ambao wanatuhumiwa kuhusika katika kuwakata kata watumishi hao na kuwachoma moto na kisa kuchoma gari lao moto katika kijiji cha Iringa Mvumi Tarafa ya Makang’wa wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Aliwataja waliouawa katika tukio hilo kuwa ni dereva wa gari walilokuwa wakisafiria, Nicas Magazini ambaye naye pia ni mtaalamu pamoja na watafiti wawili ambao ni Teddy Nguma na Faraji Mafuru.

Watafiti hao walifikwa na umauti huo baada ya kufika katika kijiji cha Iringa Mvumi Dodoma na ndipo mmoja wa wakazi wa eneo hilo akaanza kupiga kelele kuwa wamevamiwa na wanyonya damu. Aidha, mchungaji wa kanisa moja kijijini hapo akatumia kipaza sauti cha kanisa kutangaza kuwa wamevamiwa na ndipo wananchi walipoanza kuwashambulia na kuwachoma hadi kufa watafiti hao.

Katika hatua  nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amewasimamisha Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Godfrey Mnyamala na Afisa Utumishi wa Halmashauri hiyo Salum Makila kwa kosa la kupokea taarifa za utambulisho wa watafiti hao lakini hawakusambaza taarifa za ujio wa watafiti hao kwenda kwa viongozi wengine ngazi za chini kitu kinachosadikiwa kuwa ni chanzo cha vifo hivyo.

 

Comments

error: Content is protected !!