tmoja2

Yusuf Manji “apewa saa 24 kuondoka kwenye jengo la PSPF Plaza (Quality Plaza)”

666
0
Share:
Share this
tmoja2

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na Mmiliki wa Kampuni ya Quality Group amepewa notisi ya saa 24 kuanzia tarehe 2 Desemba akitakiwa kuondoka katika jengo la PSPF Plaza awali lilikuwa likifahamika kama Quality Plaza.

Notisi hiyo haikueleza sababu ya Manji kutakiwa kuondoka mara moja katika jengo hilo lakini taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa ni kutokana na malimbikizo ya kodi.

Taarifa hizo zinadai kuwa Manji anadaiwa malimbikizo ya kodi ya pango ya TZS bilioni 13. Deni hilo limetokana na mmiliki huyo kutokulipa kodi kwa miaka mingi tangu alipopangishiwa jengo hilo mali ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Notisi hiyo aliyopewa imeeleza kuwa kama asipoondika ndani ya saa 24 alizopewa, kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart & Co Ltd imepewa zabuni ya kuwaondoa kwa nguvu. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo ya udalali, Scholastica Kevela amesema kuwa tayari wameshawapa wahusika notisi hiyo na kuwataka kuondoka kwa hiari.

Uamuzi wa kuiondoa Kampuni ya Quality Group umekuja siku chache baada ya PSPF kushinda kesi iliyokuwa imefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kitengo cha Ardhi ambapo kampuni hiyo ilikuwa ikipinga kuondolewa huko.

Jengo hilo lipo katika Kitalu Namba. 189/2 kwenye Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salamaa. Makampuni yanayodaiwa kuwapo katika jengo hilo ni Quality Group Company Limited, Gaming Management Limited, Q Consult Limited, Quality Logistics Company Limited na International Transit Investment Limited ambazo zinasimamiwa na Yusuf Manji.

 

Comments

error: Content is protected !!