Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Kocha Emmanuel Amunike kuendelea kuifundisha Taifa Stars

Licha ya kutupwa nchi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2019) kwa fedheha baada ya kupoteza michezo yote mitatu ya hatua ya makundi kwa kufungwa magoli 8, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ataendelea na kibarua chake.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ammy Ninje amesema kuwa Kocha Emmanuel Amunika ataendelea kuifundisha Taifa Stars.

Amunike ambaye amewahi kuichezea Barcelona na Timu ya Taifa ya Nigeria aliteuliwa kuionoa Taifa Stars mwezi Agosti 2018, na kuiwezesha Tanzania kufuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1989.

Kocha Amunike amefanya kazi kubwa sana. Haikuwa rahisi kwa sababu alilibadilisha soka letu. Baada ya miaka 39, alikuja na kubadili mambo, na mara zote unapobadilisha vitu, unabadili mitazamo ya watu. Inachukua muda, hivyo ataendelea kuwa nasi, amesema Ninje.

Ninje alisema kuwa watatilia mkazo zaidi katika kuibua wachezaji wachanga ili kuhakikisha wanafuzu katika fainali hizo mwaka 2021.

Kwa baadhi ya wachezaji wakongwe ambao wamekuwa katika kikosi cha timu ya taifa kwa muda mrefu, haya yanaweza yakawa ndio mashindano yao ya mwisho.

Ninje amesema kwa mpira wa sasa unahitaji vijana wachanga wenye kasi na uwezo mkubwa na kwamba, kama Tanzania itafuzu tena katika mashindano yajayo, anaamini itafanya vizuri zaidi.

Bitnami