Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Mchango wa sekta ya mawasilino katika kuijenga Tanzania ya Viwanda

By John Nangi (UCC, UDSM)

Ni wazi kuwa kwa sasa serikali imejikita zaidi kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia lengo la kuwa na uchumi wa viwanda, uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Katika mkakati huo, serikali inahakikisha kuwa uchumi unakua na hii inaambatana na kuchagiza sekta binafsi kuwekeza katika viwanda katika maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha lengo linafikiwa.

Hadi sasa sekta binafsi kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kuonyesha uwezo wake linapokuja suala la kuwa na mchango chanya kwenye uchumi wa nchi. Ukichukua sekta ya mawasiliano kama moja ya mfano wa sekta binafsi, ni rahisi kuona mchango mkubwa ambao sekta hiyo imeweka kwenye ukuaji wa uchumi.

Kwa mwaka 2016 pekee mchango wa sekta ya mawasiliano pekee ulikuwa ni dola za Kimarekani 2.5 bilioni kiwango ambacho kinatabiriwa kuongezeka na kufikia dola za Kimarekani 4 bilioni ifikapo mwaka 2020, sawa na zaidi ya asilimia 6 ya pato la taifa la Tanzania (GDP).

Kama tunataka kuhakikisha kuwa mchango huu mkubwa na muhimu unaendelea kuwepo, lazima kuna mambo ya msingi katika soko yazingatiwe.

Kwa sasa kuna kampuni 8 za mawasiliano zinazofanya kazi katika soko la Tanzania. Licha ya kuwa wingi huo wa kampuni unaweza kuonekana ni jambo jema, lakini hali sivyo ilivyo.

Wataalamu wa masoko na biashara wanaweka bayana kuwa Kupunguza idadi ya kampuni katika soko la mawasiliano nchini, kutawezesha uwekezaji mkubwa wenye tija katika sekta hiyo ikiwemo uwepo wa mtaji tosha kuweka mitambo bora zaidi ya kimawasiliano, jambo ambalo litapelekea utoaji huduma bora kwa wananchi.

Mfano Kwa kuunganisha kampuni mbili au zaidi, wateja wa kampuni zitakazoungana wataweza kutumia huduma zinazotolewa na pande zote mbili. Kwa kuzingatia hilo, wateja watapata huduma bora inayoendana na thamani ya fedha yao, pamoja na kuwa na mtandao (network) kubwa na imara zaidi.

Ni muhimu kuwekwa msisitizo wa kuimarisha sekta ya mawasiliano kwa kuunganisha kampuni kama hatua mojawapo muhimu. Hatua hiyo italeta manufaa yenye tija zaidi, na kuwezesha utoaji huduma bora, pamoja na sekta kukua katika kiwango bora.

Bitnami