Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Mahakama Kuu yakataa maombi ya Tundu Lissu ya kurudishiwa Ubunge

Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali maombi ya Wakili Tundu Lissu ya kufungua shauri la kutengua uamuzi wa Spika wa Bunge, Job Ndugai kumvua ubunge.

Akitoa uamuzi huo Jaji Sirillius Matupa amesema kuwa Lissu hakupaswa kuwasilisha maombi ya kutaka uamuzi huo utenguliwe, bali alitakiwa kufungua kesi ya kupinga kufanyika uchaguzi katika jimbo hilo.

Jaji Matupa ameongeza kuwa endapo maombi hayo yakikubaliwa yatasababisha uvunjaji wa katiba kwa kuwa na wabunge wawili kwenye jimbo moja.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya uamuzi huo kutolewa Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbunge Freeman Mbowe amesema wanaheshimu uamuzi wa mahakama, lakini watarudi tena mahakamani hapo hapo haraka.

Amesema kuna njia mbalimbali za kuweza kupata haki na kwamba wanaweza kurudi mahakamani hapo, au kwenda ngazi ya juu ikiwa ni njia nyingine ya kuweza kupata haki.

Katika maombi hayo namba 18 ya mwaka 2019, dhidi ya Spika wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Lissu aliomba kibali cha kufungua shauri kupinga taarifa ya Spika ya kukoma kwa ubunge wake na mahakama iteunge taarifa hiyo

Bitnami