Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Mbowe amwambia Rais Magufuli ana nafasi ya kuweka historia ya maridhiano

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema uamuzi wake wa kuhudhuria Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika ni ishara ya kuwa kuna haja kama taifa kufanya maridhiano ili kurejesha mtengamano wa taifa letu.

Mbowe ameyasema hayo leo alipopewa nafasi ya kuzungumza katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo ndipo sherehe hizo zilipofanyika kwa ngazi ya kitaifa na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi wa serikali, sekta binafsi, pamoja na viongozi wengine wa kimataifa.

Akizungumza baada ya kutanguliwa na viongozi wengine wa upinzani, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai amesema kuwa kwa sasa nchini kuna watu wanalalamika, wengine wakidai kuumia kutokana na hali ngumu ya maisha.

Nimekuja kushiriki Sherehe za #Miaka58YaUhuru kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, mshikamano katika taifa letu. Namuomba Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia.


Mheshimiwa Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika taifa kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia. Basi Mhe. Rais tumia nafasi hiyo ukaliweke taifa katika nafasi ya utengemano.

Mbali na Mbowe, viongozi wengine waliopata nafasi ya kuzungumza na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika uwanja huo ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) ambapo amesema kuna haja ya serikali kuimarisha demokrasia hata wakati tukijiandaa kulekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Ninampongeza Rais (Dkt Magufuli) kwa kazi aliyofanya, lakini ninamuomba ajue ana jumuku la kujenga demokrasia katika nchi yetu, hasa tunapoelekea uchaguzi wa mwaka 2020.

Baadhi ya watu wameonesha kutokuunga mkono uamuzi hasa wa viongozi wa CHADEMA kuhudhuria sherehe hizo, wakidai kuwa kwa kufanya hivyo ni kuunga mkono kasoro zote ambazo zimejitokeza nchi kama vile uchaguzi wa serikali za mitaa, uhuru wa habari, na utawala bora na haki za binadamu

Hata hivyo wengine wameunga mkono kitendo hicho wakiona kwamba ni sehemu ya moja ya majukwaa ambayo wataweza kuyatumia kuzungumza na halaiki, ili kuweza kurejesha hali kama ilivyokuwa awali.

Bitnami