Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Mrembo wa Afrika Kusini atwaa taji la Miss Universe 2019

Mrembo kutoka Afrika Kusini, #ZozibiniTunzi (26) ameshinda taji la #MissUniverse2019 katika mashindano yaliyofanyika jijini Manila nchini Ufilipino.

Mrembo huyo aliwashinda wenzake wawili walioingia tatu bora ambao ni Madison Anderson kutoka Puerto Rico ambaye alikuwa wa pili, na mrembo kutoka Mexico, Sofía Aragón aliyeshika nafasi ya tatu.

Zozibini amechukua mikoba ya taji hilo kutoka kwa raia wa Ufilipino, Catriona Gray ambaye alilitwaa mwaka 2018.

Zozibini anakuwa raia wa tatu wa Afrika Kusini kutwaa taji hilo baada ya Margaret Gardiner mwaka 1978, and Demi-Leigh Nel-Peters mwaka 2017.

Mrembo huyo alizaliwa Tsolo, na alikulia katika Kiiji cha Sidwadweni nchini Afrika Kusini. Anashahada ya Uhusiano wa Umma (Public Relations) ambayo alitunukiwa mwaka 2018. Aliingia rasmi kwenye masuala ya ulimbwende mwaka 2017, ambapo mwaka huo alikuwa miongoni mwa walioingia katika kundi la warembo 26 bora waliowania taji la Miss Afrika Kusini.

Aligombea tena mwaka 2019 na kushinda ambao ushindi wake uliibua mijadala baada ya kusema katika mahojiano na kituo cha runinga kwamba watu wamekuwa wakiona kama mtu mweusi au ukishakuwa mweusi basi hauwezi kuwa mrembo, jambo ambalo si sahihi.

Nimekua katika dunia ambayo mwanamke wa kufanana nami, mwenye rangi ya ngozi kama yangu pamoja na ngozi, huchukuliwa kuwa si mrembo. Na ninadhani ni wakati sasa dhana hii kukoma. Nataka watoto wakiniangalia, wakiangalia uso wangu wajione wao pia, alisema Zozibini.

Bitnami