Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Makalapicha: Ndani ya shule yenye ada ghali zaidi duniani

Institut Le Rosey iliyo nchini Uswisi ndio shule ghali zaidi duniani ambapo ada kwa mwaka mmoja ni takribani TZS 264,518,386.

Shule hii ina kampasi mbili ambazo ni Château du Rosey iliyopo katika Manispaa ya Rolle ambayo hutumika katika kipindi cha masika na kipindi cha joto. Kampasi nyingine ni Chalets (ski resort of Gstaad) nchini humo humo ambayo hii hutumika kipindi cha baridi.

Watu maarufu waliosoma katika shule hiyo ni pamoja na Mfalme Albert II wa Ubelgiji, Shah wa Iran, Mwana-Mfalme Rainier wa Monaco, na Mfalme Farouk wa Misri.

Shule 10 zenye ada ghali zaidi Tanzania

Shule hiyo imeeleza kuwa asilimia 30 ya wahitimu wake hujiunga miongoni mwa vyuo vikuu 25 bora zaidi duniani kama vile vya  Ivy League, MIT, na Oxbridge.

Hapa chini ni picha za muonekano wa shule hiyo:

1. AerialRolleCampus.JPG
Shule hii iliyopo jirana na Mji wa Geneva imekalia eneo lenye ukubwa wa hekta 28.
2. ChateauThen
Jengo hili ambalo ni moja ya majengo ya shule hiyo lilijengwa karne ya 14, na shule hiyo ilianzishwa karne ya 19 (1880)
2. ChateauNow
Hapa ndipo wanafunzi huishi kipindi cha masika na joto.
View this post on Instagram

Начало про одну из лучших школ Швейцарии Le Rosay было чуть ниже, а сейчас о том, как попасть в школу, где на полдник подают горячий шоколад, а из окон видно Альпы и Женевское озеро😊😋 Процедура поступления стандартная, как и в любой частной школе мира, но в некоторые из них поступают вообще без проблем, а здесь есть свои особенности. Сначала на сайте школы нужно заполнить заявку📝 и приложить к ней документ об успеваемости и рекомендательное письмо от директора предыдущей школы, а также медицинский отчёт. После этого вас пригласят на ознакомительный день в школу: посмотреть кампусы, встретиться с администрацией, пройти интервью и некоторые тесты. Если приехать вы не сможете, собеседование проходит по скайпу💻 После того, как вы заплатили регистрационный взнос, ожидайте результат: ежегодно в школу принимают от 80 до 90 новых учеников, а заявок поступает около 400. То есть вполне возможно не попасть в школу, в таком случае имя ребёнка внесут в лист ожидания. На каждую страну🌎 существует квота – не более 10%. Предпочтение отдают активным,🏌⛷⛹🚴🏇 любознательным и амбициозным кандидатам. В школе два рабочих языка – английский🇬🇧 и французский🇫🇷. В возрасте 8 лет их знать не обязательно, в 12 лет надо понимать оба, с 15 лет ученик должен хотя бы на одном из этих языков говорить свободно. Самое интересное – сколько стоит💰 обучение, можно ли получить скидку и что за эти деньги предлагается – в следующем посте😊 #geneva #switzerland #travel #instatravel #traveling #picoftheday #flowers #igersgeneva #blog #igersswitzerland #architecture #flower #city #view #женева #швейцария #путешествия #путешествие #интересно #история #цветы #school #lerosey #школа #фото #город #picofday #архитектура #блог #knowabroad_школы

A post shared by Путешествия 📍Женева ШВЕЙЦАРИЯ (@knowabroad) on


11. Pool
Kuna mabwawa ya kuogelea yaliyomo ndani ya shule (ndani ya mejngo na nje ya majengo) ambayo hutumika majira ya joto
1. AerialGstaadCampus
Wanafunzi huwasili katika Kampasi Kuu ya shule mwezi Septemba, na huenda likizo fupi Oktoba na Disemba. Baada ya sikukuu ya Krismasi huenda katika Kampasi iliyopo katika Mji wa Gstaad, utamadani wa shule hiyo tangu mwaka 1916

Baada ya likizo ya Machi, wanafunzi huenda katika kampasi kuu ambapo husoma kuanzia Aprili hadi Juni. Uongozi wa shule umesema huwa ni muhimu watoto kupata likizo ya mwezi Machi, na wanaporudi huamia kwenye kampasi nyingine wakiwa na nguvu mpya tayari kuendelea na masomo.

Mwishoni mwa Juni shule hufungwa tayari kwa mapumziko ya msimu wa joto.

3. Classroom
Kuna takribani wanafunzi 400 katika shule hiyo wenye umri kati ya miaka 8 hadi 18. Wanafunzi hao wametoka katika nchi 67, na mgawanyo wa kijinsia umezingatiwa. Wanafunzi wanategemea kujua lugha zaidi ya moja, na wanaweza kujifunza hadi lugha nne ikiwa ni pamoja na Dzongkha au Swahili.

Shule hiyo hudahili wenye uwezo mkubwa kitaaluma, lakini wale pia wanaoonesha kuwa na uwezo tofauti mfano katika michezo, au wenye uwezo wa kuwa viongozi ambao wataweza kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

7. Library
Maktaba ya shule hiyo ina vitabu katika lugha zaidi ya 20
4. ScienceLab
Ngazi za elimu zimegawanyika katika madaraja manne ambayo ni juniors, cadets, jeunes seniors, na seniors. Mwanafunzi anapofikia ngazi ya juu ya sekondari (high school) anachagua kati ya
baccalauréat français au the International Baccalaureate diploma.
18. GirlsRoom
Chumba kimoja hutumiwa na wanafunzi wawili, lakini wanafunzi hao hubadilishana watu wa kukaa nao mara tatu kwa mwaka. Katika mwaka wa mwisho wa masomo, wanafunzi huishi wenyewe kila mmoja kwenye chumba chake, lakini hutumia maliwato na mwenzake mmoja.

Takribani walimu 90 kati ya 150 waliopo huishi pamoja na wanafunzi.

View this post on Instagram

5 years ago. #LeRosey #ClassOf2010

A post shared by Edward Alexander (@eddyzaquila) on

Mbali na sheria za shule kuwataka kuvaa sare za shule wanapokuwa kwenye shunguli rasmi za shule, sheria nyingine ni pamoja kuhakikisha hauweki mikono mfukoni unapozungumza na mtu, na pia endapo unayezungumza nae amekuzidi umri na amesimama, nawe unapaswa kusimama.

Darasa moja lina wastani wa wanafunzi 10, lakini sio wakati wote masomo huwa ni darasani. Hapa wanafunzi wakijifunza kuhusu mimea na kutunza bustani.
Miongoni mwa michezo ambayo wanafunzi hushiriki ni pamoja na kuendesha farasi
Bitnami