Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Nguzo 10 za kujenga uhusiano imara wa kimapenzi kwa wanaume

Kujenga uhusiano mzuri na imara wa kimapenzi, wote, mwanaume na mwanamke wanatakiwa kuchangia katika hili. Haitakiwi iwe kwamba mmoja ndio awe anajituma, halafu mwingine yeye amekaa ametulia.

Lakini kwa leo, tuzungumze na wanaume kuhusu mambo yatakayowasaidia kujenga uhusiano mzuri wa kimapenzi na mwanamke aliyenaye au yule anayetarajia kuwa nae.

1.Mwanamke akionesha nia ya kukutaka wewe, weka wazi hisia zako mapema, usisubiri muda mrefu kwani kama hutakuwa na lengo la kuwa nae utakuwa tayari umejiweka kwenye wakati mgumu zaidi.

2. Endapo tayari mwanamke yupo kwenye uhusiano na mtu mwingine usimshauri aachane na aliye naye aje kwako. Wahenga wanasema malipo ni hapa hapa duniani. Ukomtoa kwa mtu kwa nguvu, ujue kuna uwezekano na yeye akatolewa kwako kwa nguvu.

3. Hakuna kitu kama ‘friend zone’. Kwenye hiyo zone umejiweka wewe mwenyewe ukiamini kuwa siku moja atakufikiria na atakukubalia. Mwanamke akishakukataa, jifunze kukubali kukataliwa, na endelea kuparangana na maisha yako, acha kukaa sehemu moja ukiamini ipo siku yaja mambo yatakuwa tofauti.

4. Usianze uhusiano na vitu ambavyo utashindwa kuviendeleza kila mara, kwa mfano, ukianza uhusiano kwa kumpa mwenza wako zawadi kila wiki, hakikisha unaendelea hivyo hivyo, ukiona kitu hutakiweza, achana nacho.

5. Watu wengi wamekuwa wakisema, na wakiamini kwamba maelewano ndio chagizo kuu la kuwa na uhusiano imara ambao mwishoe hupelekea katika ndoa. Lakini ukweli ni kwamba, mwawasilino mazuri, au kujua mbinu za kuwasiliana kulingana na nyakati na hali ilivyo ndio nguzo kuu.

6. Uhusiano una gharama, unahitaji fedha kuhakikisha unafurahia uhusiano wako, hivyo usiko kutafuta fedha.

7. Uhusiano unahitaji muda, kujitoa, na kujituma kwa bidii. Kabla hujaamua kuwa kwenye uhusiano ‘serious’ hakikisha kuwa maisha yako yanaeleweka.

8. Usiingie kwenye uhusiano na mwanamke ukiamini kwamba utambadilisha, ni vigumu sana kumbadilisha mtu mzima. Ukimkuta anakunywa pombe na ukaamua kuwa nae, kuwa nae hivyo hivyo akiwa anakunywa, akibadilika ni heri, lakini usiwe na mawazo kuwa utambadilisha.

9. Ijali afya yako, kula vizuri, vaa vizuri, mpende na mheshimu mwenza wako. Shirikiana nae katika shughuli mbalimbali nje ya nyumbani kadiri uwezavyo.

10. Endapo kutokuelewana kukiibuka kati yenu, usipayuke wala kuthubutu kimpiga mwanamke. Jifunze kumaliza tofauti zenu kiutu uzima. Rudia pointi namba 5.

Bitnami