Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Afya: Mambo haya 8 huchangia kuwa na afya bora zaidi

Dr Frank Munuo, Dar Es Salaam

Ni wazi kuwa kila mtu anafahamu, kuweza kuwa na afya bora sio tukio la siku moja, bali ni mchakato unaochukua muda mrefu, tena unaojumuisha kujinyima, kujizuia na wakati mwingine kufanya vitu ambavyo baadhi huviona havina maana.

Wataalamu wa masuala ya afya wanaeleza kuwa ukiweza kufanya mambo haya kila siku, utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwa na afya bora:

Kulala saa 4 usiku

Najua unafahamu kuwa kutopata muda wa kutosha kulala kuna athari kubwa sana katika afya yako (huongeza uwezekano wa kupata matatizo ya moyo). Hivyo unashauriwa kupata muda wa kutosha angalau saa 7 hadi 8 kwa siku. Lakini licha ya kuweza kulala kwa muda huo wote, bado tafiti zinaonesha kuwa muda sahihi na bora zaidi ambao mtu anatakiwa kulala ni saa nne usiku, kwani kati ya muda huo hadi usiku wa manane ndio mwili hujijenga zaidi.

Kuvuta pumzi ndani na nje kwa nguvu mara kwa mara

Kutafakari (meditation) au kuvuta pumzi kwa nguvu na kuzitoa ukiwa katika mazingira yenye utulivu, kuna faida kuwa kiafya. Kwa kufanya hivyo inapunguza woga/hofu, inaratibu sukari kwenye damu, na pia kusaidia kuimarisha mfumo wa mwili kupambana na magonjwa. Unashauriwa kutenga walau dakika 10 kwa siku kwa ajili ya kutafakari or kuvuta pumzi kati ya saa saba hadi saa tisa jioni.

Kushirikiana na watu wengine

Watu wenye uhusiano mzuri na watu wengine huwa na furaha zaidi, wanaishi muda mrefu zaidi na huwa na afya bora. Kutumia sehemu ya muda wako kukaa pamoja na marafiki zako au wanafamilia husaidia kupunguza msongo wa mawazo, hivyo kukuwezesha kuwa na afya bora. Hivyo jitahidi kushirikiana na wenzako katika masuala mbalimbali yatakayokuwezesha wewe kuwa mwenye furaha, mfano kwenye shughuli za kimichezo, burudani.

Kula nuts (Karanga, korosho, almond, etc)

Ulaji wa nafaka za aina hiyi mara kwa mara katika wiki ama ziwe zimepikwa au ambazo hazijapikwa husaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza hatari ya magonjwa moyo, pamoja na kuwa na faida nyingine. Husaidia kudhibiti ongezeko la uzito wa mwili, husaidia mmeng’enyo wa chakula, kuimarisha uono, pamoja na afya ya ubungo.

Kuwa makini juu ya muda unaotumia ukiwa umekaa

Unafahamu kuwa unahitaji kuwa unafanya mazoezi mara kwa mara ili kuwa na afya bora. Lakini ukweli ni kuwa kwenda gym kwa muda mrefu hakutoshi kama unatumia muda mwingi wa siku ukiwa umekaa. Ukikaa kwa muda mrefu sana unaharibu mwili wako. Sikushauri uache kazi yako, lakini uwe unainuka mara kwa mara na kutembea kidogo, jinyooshe kwa angalau dakika 3.

Cheka

Kama umekuwa ukipuuzia kwenda au kutazama vichekesho, sasa ni wakati wa kuacha kudhani kwamba wewe umekuwa sana, na hayo mambo ni ya watoto. Unapocheka unachoma kalori kwenye mwili wako, na wakati huo huo unakua mwenye furaha. Kicheko kinapunguza sana msongo wa mawazo. Utafiti uliofanywa mwaka 2014 ulibainisha kuwa kutazama video ya vichekesho kunapunguza homoni za msongo wa mawazo na kusaidia kuimarisha kumbukumbu. Joti na wenzake ni dawa.

Pika unachokula

Kupunguza kula junkie foods au vile unavyoletewa ofisini kwako kwa kupiga tu simu, na kuanza kupika chakula unachokula, kutakusaidia zaidi kuwa na uamuzi wa nini cha kula na kiasi gani, hivyo utaweza kudhibiti uzito wako na kuepuka magonjwa mbalimbali. Kupika chakula chako kutakusaidia kwa kiwango kikubwa kuepukana na saratani, kisukari, magonjwa ya moyo, shinikizo la juu la damu.

Toka (Go out)

Tumia sehemu ya muda wako kuwa nje ya nyumba yako ambapo kutakuwezesha kupata vitamin D ambavyo ni muhimu sana katika kuimarisha misuli na afya ya akili. Utafiti uliofanywa mwaka 2015 umebainisha kuwa watu wanaopata wasaa wa kutembea maeneo yenye uoto wa asili (beach, misitu, mito, etc) huwa na mawazo hasi machache, na ubongo wao huwa na shughuli chache ambazo huweza kuwapelekea kupata matatizo ya kiakili, tofauti na wale ambao hutembea maeneo ya mijini yenye usumbufu na kero mbalimbali.

Bitnami