Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Sinema 10 zinazotazamwa sana msimu wa Krismasi

Waigizaji wengi wa sinema duniani au hata wanamuziki huwa wanapenda kutengeneza kazi ambazo ni maalumu kwa misimu fulani mfano Mwaka Mpya, Krismasi na kadhalika. Hapa chini tunakuwekea orodha ambayo kwa mujibu wa magwiji na wachambuzi wa filamu za kimagharibu, ndizo muvi 10 ambazo watu huzitazama sana msimu wa Krimasi kutokana na maudhui yake.

10. A Christmas Carol

Hii ni filamu ya zamani kabisa kwa sababu imetechezwa mwaka 1951. Muigizaji gwiji wa enzi hizo Ebenezer Scrooge (Alastair Sim), anatembelea mizimu ya zamani ya msimu wa Krismasi na picha linaanzia hapo.

9. The Muppet Christmas Carol

Mmoja ya watu muhimu kwenye filamu hii Jim Henson alifariki wakati inachezwa mwaka 1992 lakini kama una siku ya Krismasi umetulia tu nyumbani na unataka kucheki muvi zinazoendana na msimu huu basi hii ni mojawapo.

8. Bad Santa

Gwiji Billy Bob Thornton anaiba vitu kwenye duka la kuuza zawadi za Krimasi na sekeseke linaanzia hapo.

7. Miracle on 34th St.

Hii ni kesi ya jamaa ambaye alijifanya Father Christmas, ina vituko vya kufurahisha.

6. Scrooged

Mkurugenzi wa kituo cha televisheni anapotaka kufanya igizo la wazi la kuzaliwa kwa Yesu kisha mambo yanakwenda kombo.

5. Home Alone

Mtoto Macaulay Culkin kaachwa na familia yake wakati inasafiri kwenda mapumziko ya sikukuu. Huku nyuma kuna wezi wanataka kuvamia nyumba kwani wanajua hakuna mtu. Inabidi mtoto apambane kuishi hadi familia irudi na kuhakikisha nyumba pia iko salama. Filamu nzuri.4. White Christmas

Wanasema mojawapo ya matendo muhimu wakati wa Krismasi ni kusaidia wenye matatizo. Katika filamu hii ndugu wawili wanamsaidia mwanajeshi mstaafu kutopoteza nyumba yake.

3. A Christmas Story

Kutana na mtoto wa miaka 9 ambaye sikukuu hataki zawadi yoyote zaidi ya bunduki. Je ataweza kuipata?2. National Lampoon’s Christmas Vacation

Nini kinatokea familia ya ndugu wote watata watata mnapokutana kwa chakula na sherehe siku ya Krismasi?

  1. It’s A Wonderful Life

Picha ya zamani ila nzuri sana. Nyota wa sinema hii anapanga kujiua lakini ghafla msimu wa sikukuu anatokewa na malaika na kuambiwa nini hasa maana ya maisha. Kila kitu kinabadilika.

Bitnami