Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Nchi 20 za Afrika zitakazofanya chaguzi mwaka 2020

Kwa mwaka 2019 jumla ya nchi 22 za Afrika zimefanya chaguzi mbalimbali zikiwemo chaguzi za Marais, Wabunge (Wawakilishi) na chaguzi za serikali za mitaa.

Tanzania ni moja ya nchi hizo ambapo uchaguzi wa serikali za mitaa ulifanyika Novemba 24 mwaka huu.

Wakati tukielekea mwaka 2020, nchi mbalimbali zinatarajiwa kufanya chaguzi, ambapo Tanzania ni miongoni mwazo, kwani inatarajia kufanya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, uchaguzi utakaofanyika katika robo ya nne ya mwaka 2020.

Chaguzi zitakazofanyika mwaka 2020 ni pamoja na za Rais, Wawakilishi, Serikali za mitaa, na chaguzi katika majimbo kwenye nchi mbalimbali. Nchi zitakazofanya chaguzi ni:

NchiUchaguziTarehe
Burkina FasoRais na WabungeNovemba 2020
Burundi1. Rais,
2. Wabunge, Serikali za Mitaa
1. Mei 20, 2020
2. Juni 7, 2020
CameroonWabunge, Senati, Serikali za MitaaFebruari 9, 2020
Jamhuri ya Afrika ya KatiRaisDisemba 27, 2020 (duru ya pili: Februari 14, 2021)
ChadWabunge na Serikali za MitaaFebruari 2020. Ulikuwa ufanyika mwishoni mwa 2019.
ComorosWabunge Januari 19, 2020 (duru ya pili Februari 23, 2021)
MisriWabungeAprili au Mei 2020
EthiopiaWabunge, Baraza la Majimbo, Serikali za Mitaa na
Baraza la Shirikisho (House of Federation)
Mei 2020 na 2020 mtawalia
GabonSenetiMwishoni mwa 2020
GhanaRais na Wabunge 7 Disemba 2020
Guinea1. Wabunge
2. Rais
1. Februari 16 2020
2. 2020
Ivory CoastRais31 Oktoba 2020
MaliWabungeMei 2020
Namibia1. Baraza la Majimbo na Serikali za Mitaa
2. Baraza la Taifa
1. Novemba 2020
2. 2020
Niger1. Serikali za Mitaa
2. Rais na Wabunge
1. 1 Novemba 2020
2. Disemba 27, 2020 (duru ya pili 21 Februari 2021)
TanzaniaRais wa Tanzania na Zanzibar, Wabunge, Wawakilishi, MadiwaniOktoba 2020
SenegalSerikali za MitaaMwishoni mwa 2020
SomaliaWabungeDisemba 2020
ShelisheliRais Disemba 2020
TogoRais Februari 22, 2020

Baadhi ya tarehe za chaguzi hizo zinaweza kubadilika kutokana na mamlaka husika kusema kuwa tarehe tajwa zitathibitishwa.

Bitnami