Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Wanamuziki 10 wa Tanzania waliosikilizwa zaidi 2019

Programu namba moja ya kusikiliza na kupakua nyimbo mbalimbali barani Afrika, Boomplay imetoa takwimu mbalimbali za muziki nchini Tanzania kwa mwaka 2019, ambapo zinaonesha kuwa mwanamuziki Diamond Platnumz ndiye aliyeongoza kwa kusikilizwa.

Takwimu hizo zimetokana na data kutoka kwenye programu hiyo ya muziki ambayo ina watumia zaidi ya milioni 60 duniani kote, huku Tanzania kukiwa na watumiaji zaidi ya milioni 4.2.  Pia programu hiyo ina aina tofauti za nyimbo ambazo idadi yake ni zaidi ya milioni 20.

Orodha kamili ya wanamuziki 10 wa Tanzania waliosikilizwa zaidi mwaka 2019 ni;

 1. Diamond Platnumz
 2. Nandy
 3. Harmonize
 4. Rayvanny
 5. Aslay
 6. Mbosso
 7. Jux
 8. Lava Lava
 9. Joel Lwaga
 10. Vanessa Mdee

Kwa upande mwingine, nyimbo 10 kutoka Tanzania zilizosikilizwa zaidi ni:

 1. Tetetma- Ravanny Ft. Diamond Platnumz
 2. Inama- Diamond Platnumz Ft. Fally Ipupa
 3. Never Give Up- Harmonize
 4. Kanyaga- Diamond Platnumz
 5. Only You- Walter Chilambo
 6. Tamu- Mbosso
 7. The One- Diamond Platnumz
 8. Maajab- Mbosso
 9. Hazipo- Nandy
 10. Inatosha- Marioo

Albamu ya Nandy ya “The African Princess” imeshika nambari moja kwa kuwa album iliyosikilizwa zaidi 2019, huku “The Love Album” ya Jux ikishika namba mbili na kufuatiwa na “A Boy From Tandale” ya Diamond Platnumz iliyoangukia namba tatu.

Bitnami