Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

CHADEMA na ACT wataka mabadiliko matatu kuelekea Uchaguzi Mkuu

Vyama viwili vya upinzani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na ACT Wazalendo kwa kushirikiana na baadhi ya asasi za kiraia zinashinikiza kufanyika kwa mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi, wakati nchi ikijiandaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Kutokana na changamoto mbalimbali ambazo vyama hivyo pamoja na vingine vya upinzani vilikumbana navyo katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwishoni mwa mwaka 2019, sasa vinashinikiza kuwepo mabadiliko hasa kwenye haki za kisiasa kutungiwa sheria ili kuhakikisha hali kama ya kipindi kilichopita haijirudii tena.

Mambo matatu ambayo vyama hivyo vinayataka kuelekea katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ni kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi, kuwepo mfumo wa uchaguzi ambao mshindi lazima apate zaidi ya nusu (51%) ya kura zilizopigwa (simple majority), na uwezekano wa kupinga matokeo ya Urais mahakamani.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema kuwa haoni haja ya kwenda kwenye uchaguzi mkuu tungali bado na katiba ya sasa pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Msimamo wa Mnyika ambaye ni Mbunge wa Kibamba unaungwa mkono na Mshauri Mkuu wa ACT Wazalendo, Seif Shariff Hamad ambaye alisema chama hicho kitashirikiana na asasi nyingine zisizo za kiserikali kushinikiza kufanyika mabadiliko hayo.

Maalim Seif ambaye mwanasiasa mkongwe na mgombea mara tano wa kiti cha Urais visiwani Zanzibar kupitia CUF amesema kuwa yupo tayarishi kushirikiana na asasi hizo pamoja na taasisi za kidini kuleta mabadiliko.

Kutokana na kilichotokea Novemba 2019, shughuli yetu ya kwanza itakuwa ni kushinikiza kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi. Tunaamini kuwa Baraza la Vyama vya Siasa litaunga mkono mabadiliko haya, amesema Mnyika.

Bitnami