Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Hizi ni simu 5 ghali zaidi kuwahi kutengenezwa duniani

Huku baadhi wakidhani kwamba simu ghali zaidi duniani sasa ni iPhone 11 Pro (dala za Kimarekani $1,900 sawa na TZS 4.5 milioni) kuna simu duniani hapa ambazo nyingi zimetengenezwa chache kwa soko na watu maalumu ambazo bei zake huenda hujawahi kuzisikia. Hizi hutengenezwa kwa oda maalumu na huwekewa hadi madini kama dhahabu na almasi kadiri mwenye pesa anavyoagiza. Hapa chini ni simu tano ghali zaidi duniani kwa sasa. 

5. Goldvish Le Million 

Bei: Dola Milioni 1.3 za Kimarekani sawa na Shilingi Bilioni 3 za Kitanzania (yani bilioni 3 unaenda kununua simu) 

Hii wanasema kazi kubwa imefanywa kwa mkono (handmade) na ina karati 18 za white gold na karati 120 za VVS-1 gredi ya almasi. 

4. iPhone 3G Kings Button

Bei: Dola za Kimarekani Milioni 2.5 sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 5.8. Yani unatoa hiyo wanakupa simu na risiti yako ya EFD unaenda nayo nyumbani. Hii ina naksi za dhahabu za kutosha na almasi karati 138. Hapo ndipo unajua wewe na familia ya kifalme ya Saudia mnatumia iPhone ila sio sawa. 

3. iPhone 3GS Supreme Goldstriker Advanced

Bei: Dola za Kimarekani Milioni 3.14 sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 7. 

Hii imesanifiwa (designed) na magwiji wa hizo kazi wa Stuart Hughes nchini Uingereza. Huyu kazi zake ndo hizo, design wa vitu vizuri kwenye wenye pesa za kutosha. Alishawahi ku-design nyumba nzima kwa dhahabu. Hii mbali na gold za kutosha inakuja na almsi karati 7.1. 

2. iPhone 4 Diamond Rose Edition

Bei: Dola za Kimarekani Milioni 8 sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 18.1 (Hata mimi nafanya huu utafiti na kuandika ila pia wakati naona hii nimesema hivyo hivyo kama wewe, dah!)

Hii pia ka-design Mwingereza Stuart Hughes, ina dhahabu za kutosha na vipisi vidogo vidogo vya almasi kama 500 kwenye pembe zake. Pia kuna almasi vipisi 53 kwenye logo ya Apple kwa nyuma na pale kwenye home button kuna karati 7.4 za almasi ya rose.

1. Falcon Supernova iPhone 6 Pink Diamond

Bei: Dola za Kimarekani Milioni 48.5 sawa na shilingi za Kitanzania Bilioni 111.6 (Hii hatari jamani).

Hii ni simu ghali zaidi kuwahi kutengenezwa duniani na inamilikwa na mke wa Bilionea namba moja wa India Mukesh Ambani Bi Nita Ambani (halafu wewe unalia lia umeambiwa ulipe bili ya nyama kilo moja). Hii simu imetengenezwa kwa karati 24 za dhahabu na ina kipande kikubwa cha almasi nyuma ikiwa na ulinzi maalumu dhidi ya udukuzi. 

Imeandaliwa na Anna Zayonga wa CBE Dar es Salaam kwa Swahili Times

Bitnami