Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Idadi ya watalii waliotembelea mbuga za wanyama Tanzania kati ya mwaka 2009 hadi 2019

Tovuti ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa nchini imechapisha takwimu zinazoonyesha ongezeko la idadi ya watalii wa ndani na nje ambao wamekuwa wakitembelea mbuga na hifadhi za taifa nchini kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2019. Takwimu zinaonyesha kuwa watalii toka nje waliongezeka kuanzia mwaka wa fedha 2009/10 hadi mwaka 2011/12 kabla ya kuanza kushuka kuanzia 2012/13 hadi 2015/16 na kisha kuanza tena kuongezeka kuanzia 2016/17 hadi mwaka 2019 uliomalizika. Kwa upande wa watalii wa ndani idadi ilikuwa ikiongezeka kuanzia mwaka 2009/2010 hadi 2015/16 kisha ikashuka 2016/17 kabla ya kupanda tena 2017/2018 hadi hivi sasa.

Hapa nchini ni orodha hiyo ambayo kolamu ya kwanza inaonyesha mwaka wa fedha ambao idadi husika ilirekodiwa, kolamu ya pili inaonyesha watalii kutoka nje, kolamu ya tatu inaonyesha watalii wa ndani na kolamu ya mwisho inaonyesha jumla.

Tanzania ina vivutio lukuki ambavyo vimekuwa vikihusudiwa na wageni na wenyeji mwaka hadi mwaka ukiwemo Mlima Kilimanjaro na Serengeti. Kukua kwa kipato kunaelezewa kuwa pia ni moja ya sababu zinazokuza utalii wa ndani ambapo idadi ya Watanzania wanaokwenda kutembelea mbuga za wanyama nayo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Chanzo: TANAPA

Bitnami