Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Ifahamu mishahara ya wachezaji wa Aston Villa

Jana Jumatatu Januari 20 Mbwana Ally Samatta aliandika historia kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kusajiliwa kucheza katika Ligi Kuu ya Soka Uingereza (EPL) moja kati ya Ligi bora zaidi za soka duniani. Samatta anajiunga na Villa timu hiyo ikiwa na kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha haishuki daraja kutoka na nafasi yake ya sasa katika msimamo wa EPL. Kulingana na mtandao maarufu wa mishahara ya wanamichezo wa SpotRac, hapa chini ni baadhi ya mishahara ya wachezaji mbalimbali wa sasa wa kikosi cha Aston Villa katika paundi za Uingereza (paundi 1 ni wastani wa shilingi 2,800 za kitanzania). Hakuna taarifa nyingi kuhusu mkataba wa Samatta lakini atakuwa mmoja ya wachezaji ghali zaidi katika timu yake hii mpya. Mtandao wa Birmingham Mail unaeleza kuwa moja ya kazi na sababu za kusajiliwa Samatta ni kuziba pengo la Mbrazil Wesley Moraes ambaye kwa sasa ni majeruhi kwa muda mrefu. Inakadiriwa kuwa Moraes hulipwa Paundi 60,000 kwa wiki (sawa na shilingi za Kitanzania milioni mia moja sitini na nane).

Bitnami