Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Maoni: Kuelekea Tanzania ya viwanda yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025

Na Ndekana Utouh, Dar Es Salaam via habari@swahilitimes.com

Mwanzo wa mwaka huu ni kengele ya miaka mitano kuelekea 2025 mwaka ambao Tanzania ilipanga kuwa imefikia lengo lake la kuwa nchi ya uchumi wa kati, ya viwanda.Dira hii ambayo Tanzania ilianza nayo mwanzoni mwa karne hii ya 21 inatambulika kuwa ni moja ya malengo makubwa ya Rais Dkt John Magufuli. 

Mpango ni kuwa na nchi yenye amani, kuondoa rushwa na wakati huo huo kujenga uchumi imara. Katika kufikia malengo haya, kuhakikisha kwamba mazingira ya uwekezaji nchini yanabaki kuwa bora ni moja ya jambo muhimu kabisa.

Mpaka wakati naandika makala hii fupi, sekta nyingi nchini zimefaidika na uwekezaji. Chukulia kwa mfano sekta ya mawasiliano ya simu ambayo kwa pamoja imewekeza zaidi ya shilingi trilioni 6 za Kitanzania hapa nchini.Uwekezaji mkubwa kama huu ni muhimu sana na umeleta faida nyingi zinazobadili maisha ya wengi nchini katika mawasiliano, kutuma na kupokea fedha, afya na mengine mengi.  

Ili kuendelea kuona faida za sekta binafsi ikiwekeza katika uchumi wetu lazima kuendelea kuhakikisha mazingira ya uwekezaji yanabaki kuwa bora kwa wawekezaji wa sasa na wajao. Hii italihakikishia taifa mazingira bora ya kuendelea kuvuna faida za uwekezaji na Watanzania kuendelea kufurahia matunda yake. 

Bitnami