Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Karibu asilimia 100 ya watumiaji wa intaneti kwa simu nchini hutumia kupitia vifurushi (bando)

Huduma ya intaneti imekuwa jambo muhimu kwenye maisha yetu ya kila siku. Iwe ni kuwasiliana, kusoma habari, kupakua muziki, filamu na kadhalika intaneti imekuwa ni hitaji kubwa kwa sasa. Takwimu zinaonyesha kwamba nchini Tanzania asilimia kubwa ya watu wanatumia intaneti kupitia simu zao za mkononi tofauti na miaka michache ya nyuma ambapo watu ilibidi waende kwenye maeneo maalumu yenye kompyuta na yanayotoza fedha kwa muda unaotumia intaneti kupitia kompyuta husika (internet cafes).

Kutokana na umuhimu wake kwenye maisha yetu ya kila siku, bei ya intaneti sasa imekuwa jambo muhimu. Takwimu zinaonyesha kuwa takribani asilimia 99.97 ya watumiaji wa intaneti kupitia simu hujiunga na vifurushi mbalimbali (bando) kuendana na mahitaji yao. Hii ni karibu asilimia mia moja. Mfano mwanafunzi atajiunga na kifurushi cha mwanafunzi, mpenda chats atajiunga na kifurushi kinachompa nafasi na MBs zaidi ku-chat, na kadhalika.

Kinachoonekana kwa uwazi hapa ni unafuu mkubwa wa bei ya MB 1 pale mhusika anapotumia vifurushi badala ya kufanya matumizi ya salio lake kupereuzi intaneti bila kujiunga na kifurushi. Unafuu huu ndio hasa unawafanya karibu asilimia mia moja ya watumiaji kutumia vifurushi hali inayoweza kutafsiriwa kuwa kwa sababu kila mtu hupenda kitu bora kwa bei bora, vifurushi vimekuwa chaguo sahihi.

Kampuni nyingi za simu huhimiza wateja wake kujiunga na vifurushi kulingana na mahitaji yao ili kupata MBs nyingi zaidi kwa gharama nafuu na njia mojawapo ya kufanya wateja kujiunga ni ile ya kuweka gharama kubwa kwa MB kama hujajiunga ambayo kwa hakika imesadia wengi kutumia vifurushi. Hapa chini ni takwimu za TCRA (Septemba 2019) kuonyesha bei kwa kila mtandao nchini Tanzania pale unaponunua kifurushi chenye mchanganyiko wa dakika, SMS na data (MBs). Hii ni bei (bila kodi) ya mchanganyiko wa SMS 1 + dakika 1 ya muda wa maongezi + MB 1

Ndani ya Mtandao (on-net)

Airtel TZS 41

Halotel TZS 21

Tigo TZS 27

Vodacom TZS 31

Zantel TZS 58

Nje ya Mtandao (off-net)

Airtel TZS 54

Halotel TZS 42

Tigo TZS 33

Vodacom TZS 52

Zantel TZS 62

Sehemu ya taarifa ya TCRA kuhusu gharama kwa kila mtandao.

Soma zaidi hapa.

Bitnami