Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Waziri Dkt Kigwangalla: “Kuna watu walipanga njama za kuniua.”

Mapema leo Waziri wa Maliaasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini ameeleza kwa kwa ufupi kupitia akaunti yake rasmi kwenye mtandao wa Instagram kwamba wako watu wanaopanga kumchafua ili aondolewa katika nafasi ya Uwaziri. Asema kwamba matukio ya hivi karibuni ya moja ya magazeti nchini kuibua tuhuma zisizo na msingi dhidi yake ni mwendelezo wa kazi zinazofanywa na watu hao.

Katika mtandao wa Instagram ameandika:

“Sikusudii kufanya press conference. Watu wengi wamenishauri niishie hapa. Team yangu imefanya

kazi nzuri, imenipa uthibitisho wa majina ya wanaotaka nichafuliwe ili niondolewe uwaziri. Bahati

mbaya hakuna cha kunichafua nacho, wanapika hadithi za kitoto na kurudia tu. Walidhani ningekaidi

maelekezo ya Mhe. Rais juu ya mgogoro wa ndani ya Wizara yetu ili Rais achukie aniondoe,

wakakwama. Sikukaidi. Wakaona wafanye mwendelezo kupitia gazeti, sijataka kujibishana nalo,

tutakutana mahakamani ambapo mbivu na mbichi zitajulikana, ukweli utawekwa wazi na rekodi

itakaa sawa. Sijashangaa kuwa wahusika ni wale wale wa kipindi kilichopita. Hakuna jipya. Sababu ni

deal yao binafsi, ambayo haitekelezeki bila ridhaa ya Waziri, na bahati mbaya kwao Waziri ni mimi;

walitamani nisiwepo watafune pesa za serikali vizuri, wamekwama. Tutaendelea kudhibiti kimya

kimya. Kwa wanaokumbuka wakati nimelazwa ICU na baadaye wodini, ilikuwa ngumu sana

kunitembelea na kuniona. Paliwekwa ulinzi mkali sana na watu wote walizuiliwa kuingia isipokuwa

kwa kibali cha Ikulu, hadi Mawaziri wenzangu hawakuruhusiwa. Nilishangaa sana lakini niliambiwa

ndiyo hivyo. Baadaye nikaja kujua kuwa kuna watu walipanga njama za kuniua na hiyo ingeweza

kuwa fursa kwao kunimalizia. Baada ya kuteuliwa tu Wizara hii kulizuka mtafaruku mkubwa sana juu

ya usalama wangu, nilifuatiliwa kila kona mpaka serikali ikanipa walinzi, nilibisha kwa kuwa sipendi

attention sana lakini nililazimishwa na kuambiwa nipo kwenye ‘threat’! Sikuwa na option. Nilianza

kuishi kwa hofu na mashaka sana. Hivyo, baada ya ajali na yaliyotokea kutokea nililazimika kuwa

makini zaidi. Imani yangu kwa kila mtu ilipungua. Nikawa ‘alert’ wakati wote. November 2019

nililetewa taarifa za kutisha, nikaongeza umakini. Team yangu imenisihi nisiweke majina hadharani

na kwamba wanawafuatilia wahusika kwa ukaribu na watazijulisha mamlaka kwa hatua stahiki zaidi.

Watu wa karibu sana na mimi nimewapa mpango na taarifa zote na wanajua cha kufanya endapo

chochote kitanitokea. Kuna mbinu nyingi za mapambano. Tuendelee tu!”

Bitnami