Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Taarifa ya Serikali ya Sweden kubadili mkakati wake wa ushirikiano wa kimaendeleo na Tanzania

**Mwanzo**

Serikali ya Sweden yabadili mkakati wake wa ushirikiano wa kimaendeleo na Tanzania 

Februari 3, 2020

Serikali ya Sweden imeanza kutumia mpango mkakati mpya wa miaka mitano wa kimaendeleo kati yake na Tanzania. Mkakati huo mpya unatofautiana na ule wa zamani kwa namna kwamba unapunguza kiwango cha misaada kwa kuzingatia maendeleo hasi kwenye masuala yanayohusu demokrasia nchini Tanzania. Mkakati huu mpya unamaanisha kwamba Sweden itaimarisha nguvu zake za kiushirikiano na kuweka kipaumbele kwenye maeneo kama haki za binadamu, demokrasia, usawa wa kijinsia, mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa. 

Katika miaka ya hivi karibuni maendeleo hasi yameonekana nchini Tanzania hasa kwenye eneo la haki za binadamu na demokrasia. Kupitia mpango huu mpya, maeneo ya ushirikiano kati ya wadau kwa pamoja yatachangia kuimarisha mazingira ya demokrasia na maendeleo ya demokrasia nchini Tanzania. 

“Mkakati huu mpya unajikita katika makundi yaliyo pembezoni na walinzi wa demokrasia na hili ndilo mkakati huu unakwenda kufanya. Sweden itafanya kazi na serikali ya Tanzania katika maeneo ambayo yataleta ahueni kubwa kwenye maisha ya watu masikini zaidi. Katika wakati huo huo, ili kuhakikisha maendeleo ya kidemokrasia tutaimarisha kuunga mkono taasisi za kiraia na sekta binafsi,” anaeleza Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, Peter Eriksson.

Kazi ya Sweden katika sekta ya elimu itaendelea. Mkakati huu unaendelea na kazi na mafanikio ambayo tayari yamepatikana katika miaka ya karibuni na unakusudia kuboresha elimu shirikishi, bora na ambayo inawapa kipaumbele watoto kike na wale waliopata watoto katika umri mdogo.

Sweden itaendelea kuunga mkono uwezeshaji wa wanawake kiuchumi na kisiasa, eneo ambalo msaada katika afya ya uzazi na haki zake pia vina mchango mkubwa. 

Sweden itaendeleza juhudi zake kuchangia mazingira bora kwa makundi yaliyo katika hali hatarishi, hasa wanawake na vijana. Maeneo mengine muhimu katika mkakati huu ni kusaidia katika matumizi ya nishati sahihi, ushiriki wa wanawake katika kufanua maamuzi kwenye namna ambayo rasilimali zinapaswa kutumika. 

“Matumizi ya rasilimali nchini Tanzania yameongezeka. Wakati huo huo, mabadiliko ya tabia nchi yanapelekea kwenye kilimo ambacho kinategemewa na watu wengi masikini. Hii ndio sababu ni muhimu kwamba Sweden lazima iongeze shughuli zake katika eneo hili kwa mfano katika ukulima unaojali mabadiliko ya hali ya hewa na matumizi endelevu ya rasilimali kama uhifadhi na uhuishaji wa uoto,” anaeleza Bw. Eriksson.  

Mkakati huu mpya utatoa Krona Bilioni 3 za Kiswidi katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2020 hadi 2024.

**Mwisho**

Makala halisi ya Kiingereza inapatikana hapa. Makala hii ya Kiswahili imetafsiriwa na Swahili Times. 

Bitnami