Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Wateja wa Vodacom kufurahia mawasiliano ya kiwango cha juu baada kampuni ya Vodacom kuboresha menu na huduma zake

Wateja wa Vodacom kufurahia mawasiliano ya kiwango cha juu baada kampuni ya Vodacom kuboresha menu na huduma zake 

  • Menu rahisi, na iliyoko wazi zaidi, 
  • Bando mpya ya siku 3 za sauti na data ambazo zinatoa thamani zaidi kwa wateja. 

Tarehe 15 Februari 2020 Dar es Salaam. Kampuni ya teknolojia ya mawasiliano inayoongoza Tanzania Vodacom Tanzania PLC leo imetangaza kupunguza bidhaa zake katika menu yake kwa asilimia 75 katika jitihada za kuboresha huduma kwa wateja. 

Akiongea wakati wa kutoa tangazo hilo Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Vodacom Bi Harriet Lwakatare amesema kwamba hatua hii ni mwitikio wa mahitaji ya wateja ambao walipendekeza kuwa menu iliyopita ilikuwa ni ngumu kuifuata kutokana na kuwepo kwa chaguzi nyingi. 

“Tunakusudia kutoa huduma rahisi na zilizoko wazi kwa wateja wetu na menu hii iliyorahishwa inahakikisha kwamba wateja wetu wanaweza kwenda haraka na kwa hatua chache kufikia huduma wanayoihiji” alisema. 

Wateja wa Vodacom wanapata huduma na bidhaa za kampuni kupitia mifumo mbalimbali ikiwemo USSD code ya*149*01#, app ya Vodacom na tovuti ambazo sasa vinatoa chaguzi bora zaidi. 

Kwa upande wake, Bi Linda Riwa, Mkurugenzi wa Idara ya Bishara  wa kampuni ya Vodacom amesema “Sisi pia tumesikia kile ambacho wateja wetu wanahitaji. 

Nina furaha kubwa kutangaza kampeni yetu mpya  ya ‘Wajanja hatuzimi data” inayowapa wateja wetu unafuu katika matumizi ya intaneti pamoja na uzinduzi wa bando mpya ya Jimwage ambapo wateja wanaweza kupata GB 3 kwa siku 3 kwa shilingi 2,500 tu. Hii inawezesha kila mtu kutumia mtandao wetu Supa  kwa bei nafuu na kufaidika zaidi.

“Pia tumeboresha huduma yetu ya sauti  ili kuwezesha wateja wetu kuongea na wapendw wao bila kujali mtandao gani unayoipigia au gharama za ziada kwa mfano huduma yetu ya cheka iliyoboreshwa  inatoa dakika 25 kwa shilingi 500 kupigia mitandao yote”

Akizungumza kuhusu bidhaa za Data, Mkuu wa Idara ya bidhaa za wateja Celvin Mmasy alisema, “uzinduzi wa bidhaa mpya za data zinawezesh kila Mtanzania kuungnishwa kupitia mtandao Supa wa Vodacom yenye uhakika, sidi kubwa kwa bei hafuu”.

Mwisho

Bitnami