Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Taarifa ya hali ya Watanzania 420 waliopo Wuhan, China

Serikali imewatoa hofu Watanzania hususan wazazi, ndugu na jamaa wa wanafunzi takribani 420 walioko katika Jimbo la Hubei, mjini Wuhan, China, ambapo ndio kitovu cha maambukizi ya virusi vya homa ya Corona (COVID-19) kuwa hadi sasa hakuna mwanafunzi au Mtanzania yeyote aliyebainika kuambukizwa virusi hivyo.

Aidha, serikali kupitia wizara ya mambo ya nje imesema haina mpango wa kuwaondoa ama kuwasafirisha wanafunzi hao kuwa wako katika uangalizi maalumu (quarantine) nchini humo kutokana na serikali kuheshimu masharti na mahitaji ya karantini hiyo yanayozuia mtu yeyote kutoka ama kuingia katika mji huo kwa kusudi la kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

Uamuzi huo unatokana na taarifa za kitabibu zinazobainisha kutokea milipuko ya homa ya virusi hivyo katika mataifa ambayo awali yaliwaondoa wananchi wao wakati wa mlipuko na kusababisha kusambaa kwa virusi hivyo na kuleta madhara zaidi kwa mataifa hayo.

Serikali imesema imeendelea kuzipatia ufumbuzi changamoto za wanafunzi hao ikiwa ni pamoja na kuwapatia vifaa vya kinga ikiwemo viziba pua (Masks) na sabuni maalum za kunawa mikono (Disinfecants) pamoja na kusaidia utatuzi wa mahitaji ya lazima pale inapojitokeza.

Serikali pia inakamilisha mpango wa mawasiliano ya moja kwa moja kwa njia za simu (hotline) zitakazotumiwa na wataalamu wa saikolojia (psycho-social support) kwa ajili ya kuwapatia ushauri nasaha wanafunzi na wazazi wakati juhudi za kudhibiti mlipuko huo zikiendelea.

China ilikumbwa na mlipuko wa homa ya corona (the novel coronavirus- 2019-nCoV) ambavyo jina lake rasmi kwa sasa kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO) ni COVID – 19 kuanzia Januari, 2020.

Bitnami