Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Uchaguzi Tanzania kuwa huru na haki- Prof. Kabudi

Tanzania imeihakikishia jumuiya kimataifa kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 utakuwa wa uwazi, huru na wa haki, na kwamba wananchi watapewa nafasi ya kutimiza wajibu wao.

Akihutubia katika Kikao cha 43 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa linaloendelea Geneva nchini Uswisi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema Tanzania itaalika waangalizi kushuhudia namna Watanzania wanavyotekeleza moja ya haki zao za msingi katika suala la kidemokrasia kwa kuchagua viongozi wao.

Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa Tanzania inaheshimu na itaendelea kuheshimu haki zote binadamu, na kwamba hatua ya Bunge la Tanzania kufanya mabadiliko ya sheria za vyama vya siasa, sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali na ile ya vyombo vya habari ina lengo la kuimarisha uwajibikaji na uwazi pamoja na kuhakiskisha misingi na tunu za Taifa zinaheshimiwa na kuendelezwa.

Ameongeza kuwa madai yanayoishutumu Tanzania kukiuka haki za binadamu ni propaganda na haswa zinatokana na hatua kali zinazochukuliwa dhidi ya rushwa, ubadhirifu wa mali za umma, madawa ya kulevya, uzembe katika ofisi za umma, pamoja na hatua zinazochukuliwa kulinda rasilimali na maliasili ya Tanzania kwa manufaa ya Watanzania.

Wakati huo huo, Waziri Kabudi amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland, mazungumzo yaliyolenga masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na mradi ambao Jumuiya ya Madola umeufanya kuhusu Tanzania.

Bitnami