Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Waliosambaza picha za ubovu wa barabara wamehujumu uchumi: RC Gambo

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameagiza kukamatwa na kuhojiwa kwa watu waliosambaza picha zinazoonesha ubovu wa barabara za Hifadhi ya Ngorongoro kwa maelezo kuwa kitendo hicho kimechafua taswira ya nchi.

RC Gambo ameeleza kuwa serikali haikatazi mtu kuripoti tatizo, lakini liripotiwe kwenye mamlaka husika, kwani ndizo zenye uwezo wa kufanya mabadiliko.

Amesema watu hao waliosambaza picha kwenye mitandao ya kijamii wamehujumu uchumi wa nchi kwa kuchafua taswira yake, huku akieleza kuwa matatizo kama hayo hayapo Tanzania pekee, lakini Wananchi wa nchi nyingine hawayaoneshi kutokana na kuwa wazalendo.

Msikilize RC Gambo hapa chini akitoa agizo hilo:

Bitnami