Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Makamu Mwenyekiti wa CCM aliwekewa sumu: Kamanda Mambosasa

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema baada ya kufanya uchunguzi wamebaini kuwa ndani ya mwili wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula kulikuwa na sumu.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Kamanda Lazaro Mambosasa amesema kuwa Februari 28 mwaka huu mara baada kikao cha chama hicho kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za Lumumba jijini Dar es Salaam, Mangula alianguka na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

“Baada ya uchunguzi, jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na taasisi mbalimbali tumebaini kuwa ndani ya mwili wa Mzee Mangula kulipatikana na sumu,” amesema Mambosasa.

Aidha, ameongeza kuwa uchunguzi kuhusu tukio hilo kuhusu namna sumu ilivyoingia mwilini unaendelea na kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kuhusika kwa namna yoyote na tukio hili bila kujali anatokea chama gani, taasisi gani, au awe raia au sio raia wa Tanzania.

Mambosasa amewataka wananchi kujiepusha na vitendo hivyo ambavyo tu si kwamba ni vya kinyama, bali pia vinakiuka sheria za nchi.

Bitnami