Header Ad

zinazosomwa zaidi

Most Viewed

Serikali inatekeleza ajenda za upinzani- Prof. Lipumba

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) amewakosoa wanasiasa wanaopinga kila jambo linalofanywa na serikali na amebainisha kuwa serikali ya awamu ya tano imetekeleza vizuri mambo mengi yaliyokuwa yakisemwa na vyama vya upinzani.

Prof. Ibrahim Lipumba ameyasema hayo akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam katika mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli ambapo ameongeza kuwa si sawa kwa vyama upinzani kupinga jambo vililotaka litekelezwe na linatekelezwa, mfano kurekebisha sheria ya madini na kupambana na rushwa.

Katika hatua nyingine Lipumba amempongeza Rais Magufuli kwa ahadi yake kuwa uchaguzi mkuu utakuwa huru na wa haki, na amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kupambana na rushwa, kudhibiti matumizi ya serikali, kulinda na kutumia vizuri rasilimali za Taifa, kuboresha elimu, na kuimarisha uchumi.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania wote kuweka uzalendo mbele, kudumisha amani na utawala bora, na amewataka wanachama wote wa CUF kujiandaa kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo.

Bitnami