Alichosema Wema Sepetu baada ya video yake aki-kiss kusambaa mitandaoni

385
0
Share:
Share this
  • 377
    Shares

Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu ameomba msamaha watu mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bodi ya Filamu Tanzania baada ya video yake akibusiana na mwanaume kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Wema ameomba msamaha wakati akizungumza na vyombo vya habari leo ambapo amesema anajutia kitendo hicho na kwamba anawaomba msamaha wale wote aliowakwaza na zaidi mama yake mzazi.

Amesema kuwa wapo watu wengi wanaomtazama yeye kama kioo cha jamii, na hivyo kusambaa kwa video hiyo ambayo amesema hataki kutupa lawama kwa mtu yeyote, anajua kutakuwa kumewakwaza wengi.

Licha ya Wema kuchukua hatua hiyo, watu wameona kutokujali kwa kile wanachodai kuwa sio mara yake ya kwanza kufanya kitendo kama hicho na kujitokea na kuomba radhi huku akiahidi kutorudia.

Kwa siku za hivi kumekuwa na matukio kadhaa ya uvunjifu wa kimaadili yanayowahusisha wasanii wa filamu na muziki nchini Tanzania jambo ambalo linaonesha kuwakwaza wadau na hasa mashabiki wa tasnia hiyo ya burudani.

Kabla kusambaa kwa video hiyo ya Wema, zilianza kusambaa picha akiwa na mwanaume huyo ambaye amesema kuwa ni mume wake mtarajiwa.

 

Comments

error: Content is protected !!