Aliyewanunua Madiwani Arusha akimbilia kwa mganga

410
0
Share:
Share this
CMTL Group

Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nassari amesema kuwa mmoja wa watuhumiwa wa rushwa ya ununuzi wa madiwani mkoani Arusha ameleta mganga wa kienyeji ili kusaidia kulinda ajira yake.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa kiongozi huyo, ameandika, “Mmoja wa watuhumiwa wa rushwa ya ununuzi wa madiwani Meru aishie maeneo ya Mukidoma Usa-River ameleta mganga toka Kanda ya Ziwa, na yupo nyumbani kwake.”

Katika taarifa hiyo, Nassari amesema kuwa, mganga huyo ameletwa na mama wa mtuhumiwa kwa lengo moja la kumsaidia mtuhumiwa huyo asipoteze ajira yake.

Juma lililopita, Nassari akiwa ameambatana na wabunge wengine wa CHADEMA waliwasilisha TAKUKURU kile walichosema kuwa ni picha za video zikionyesha namna madiwani wa CHADEMA katika Halmashauri ya Meru walivyonunuliwa na kupelekea kujiuzulu nyadhifa zao na kutimkia CCM.

Miongoni mwa watu wanaotuhumiwa kuhusika katika kitendo hicho ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru.

Licha ya tuhuma za ushahidi huo kutolewa, baadhi ya madiwani waliojiuzulu wamekanusha tuhuma za kununuliwa na kumtaka Nassari kuwaomba msamaha, vinginevyo watakwenda mahakamani kuwashtaki kwa kuwachafua.

Madiwani hao kwa nayakati tofauti wamenukuliwa wakisema kwamba, hawakujiuzulu kwa sababu wamenunuliwa, lakini walijiuzulu ili kumuunga mkono Rais Magufuli kwa namna anavyotenda kazi katika jitihada zake za kuwatumikia wananchi.

Comments

error: Content is protected !!