Amber Rutty, James Delicious wasomewa mashtaka yanayowakabili

512
0
Share:
Share this
  • 445
    Shares

Msanii Amber Rutty pamoja na mpenzi wake ambaye jina lake halijajulikana, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo ambapo wamesomewa mashtaka juu ya kesi inayowakabili kuhusu video zenye maudhui ya ngono.

Akiwa mahakamani hapo, Amber Rutty amesomewa mashtaka mawili, moja la kukubali kuingiliwa kinyume na maumbile na kosa la pili ni kusababisha kusambaa kwa picha za ngono.

Wakati Amber Rutty akikumbana na hayo, kijana mmoja ambaye hutumia jina la James Delicious katika mitandao ya kijamii, naye amepandishwa mahakamani na kusomewa shtaka moja la kusambaza video za ngono mtandaoni. Mtuhuiwa huyo amekana shtaka hilo.

Endapo watuhumiwa hao watatiwa hatiani kwa makosa hayo, wanaweza kufungwa kifungo cha maisha jela au kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mujibu wa Kanuni za Adhabu za Mak0sa ya Jinai.

 

 

Comments

error: Content is protected !!