Baada ya kuondoka WCB, Rich Mavoko aweka wazi uhusiano wake na Diamond Platnumz

524
0
Share:
Share this
  • 337
    Shares

Msanii wa muziki Bongo, Rich Mavoko amesema hana tatizo lolote na Diamond Platnumz licha ya kuondoka kwenye lebo ya WCB.

Muimbaji huyo kwenye Mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema kilichotokea kati yake na lebo hiyo sio ugomvi bali ulifika mwisho wa biashara yao, hivyo sasa wapo vizuri pamoja na uongozi mzima wa lebo hiyo.

Katika hatua hatua nyingine Rich Mavoko amesema kuwa maneno yanayosikika mwanzoni kwenye video ya wimbo Ndegele hayawahusu WCB kwani walikuwa wanataka tu kuvuta attention ya mashabiki ila kuhusu kuwa ni diss kwa lebo sio kusudio lao kabisa.

Mwaka 2016 Rich Mavoko alijiunga na WCB, wimbo wake wa kwanza kutoa chini ya lebo hiyo unakwenda kwa jina la Ibaki Stori, kisha Kokoro na nyinginezo, pia ameweza kufanya kazi na wasanii wengine nje ya WCB kama Fid Q, Stereo, Nay wa Mitego, Lulu Diva na wengine.

Comments

error: Content is protected !!