Baba apandishwa kizimbani kwa kumbaka binti yake

544
0
Share:
Share this

Sadick Jafari mkazi wa Manispaa ya Tabora amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Tabora Mjini, kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia ujauzito binti yake mwenye umri wa miaka 16 jambo ambalo limesababisha kukatisha kwa masomo ya binti huyo.

Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Shule, Kata ya Kiloleni, Manispaa ya Tabora, Christina Kitundu aliieleza Mahakama kwamba mtuhumiwa Sadick Jafari ambaye amekuwa akiishi na binti yake katika nyumba yenye chumba kimoja na sebule amekuwa akifanya tendo la ndoa na binti yake wakati binti huyo akiwa amelala.

Christina aliendelea kuieleza Mahakama kuwa baada ya mtuhumiwa kubaini kuwa amekwisha msababishia binti yake ujauzito aliamua kumsafirisha ikiwa ni mpango wa kuficha ukweli wa mambo aliyokuwa anayafanya.

Afisa Mtendaji  wa mtaa huo, Christina ambaye alikuwa na jukumu la kufuatilia watoto wanaokatisha masomo kwa sababu mbalimbali, alilazimika kuchukua hatua za kumrudisha binti huyo mkoani Tabora na ndipo alipojiridhisha kwamba ni mjamzito na siku chache baadae akajifungua mtoto wa kiume.

Ushahidi wa awali uliotolewa na binti huyo ambaye aliieleza mahakama kwamba baba yake mzazi amekuwa akimbaka mara kadhaa majira ya usiku tangu mwezi Januari 2017 akiwa nyumbani na alimtishia kumdhuru endapo atasema jambo hilo mbele za watu.

Hata hivyo mtuhumiwa Sadick Jafari amekana mashtaka hayo na kurudishwa mahabusu huku kesi hiyo ikitarajiwa kuendelea kuusikiliza ushahidi wa Daktari mnamo Disemba 19 mwaka huu.

Comments

error: Content is protected !!