Baba yake Vicent Kompany achaguliwa Meya wa kwanza mweusi Ubelgiji

317
0
Share:
Share this
  • 716
    Shares

Baba mzazi wa Vicent Kompany ambaye ni nahodha wa Klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza, Pierre Kompany ameweka historia baada ya kuwa raia wa kwanza mweusi nchini humo kuchaguliwa kuwa meya.

Pierre Kompany ambaye alifika nchini Ubelgiji mwaka 1975 akitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kama mkimbizi, amechaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Ganshoren katika jiji la Brussels.

Alijiingiza kwenye siasa mwaka 2006 ambapo alichaguliwa kuwa diwani, na kupata nafasi ya kuingia katika Bunge la Mkoa wa Brussels mwaka 2014.

Mzee huyo anafahamika zaidi kupitia mwanae Vicent Kompany ambaye ni nahodha wa Man City na mchezaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji. Kaka wa Vicent, Francois anaichezea klabu ya KSV Roeselare ya Ubelgiji.

Watoto wake hao wawili walimpongeza baba yao kwa hatua hiyo na kuweka historia nchini humo.

 

Comments

error: Content is protected !!