Benki 5 zilizozuiwa na BoT kufanya biashara ya kubadilisha fedha

470
0
Share:
Share this
  • 502
    Shares

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezifungia kwa muda wa mwezi mmoja benki tano kutojihusisha na baishara ya ubadilishaji wa fedha za kigeni kutokana na kukiuka kanuni zinzoongoza biashara hiyo.

Hatua hiyo ni muendelezo wa njia za udhibiti unaofanywa na BoT dhidi ya wanaofanya biashara hiyo, kwani hivi karibuni maduka kadhaa ya kubadilishia fedha hiyo jijini Arusha yalikaguliwa na mengine kufungwa baada ya kubainika kuwa na kasoro mbalimbali. Mbali na maduka hayo kufungwa, pia baadhi ya wahusika ambao idadi yao haijafahamika walikamatwa katika operesheni hiyo.

BoT imesema kuwa benki zilizofungiwa zimekiuka sheria ama kwa kutumia viwango vya kubadilishia fedha vilivyopo nje ya soko, au hawakuwasilisha taarifa za mauzo waliyofanya kama ambavyo sheria inataka.

Benki zilizofungiwa kufanya biashara hiyo kunazia Novemba 23, 218 ni Barclay Bank Tanzania, Exim Bank, UBA Bank, BancABC na Azania Bank.

Stanley Kafu, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano cha Exim Bank alithibitisha benki kuzuiwa kufanya bishara hiyo na BoT, kutokana na kucheleweshwa kuwasilisha hesabu za mauzo yao.

Hata hivyo ameeleza kuwa, zuio hilo kwao linahusu dola ya Marekani na shilingi pekee, na kwamba wanaruhusiwa kufanya biashara ya kubadilisha fedha nyingine.

Imeelezwa kuwa BoT imekua ikichukua hatua hizi kutokana na kuzidi kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani ambayo sasa ni zaidi ya TZS 2,300.

Comments

error: Content is protected !!