Bosi wa Clouds, Joseph Kusaga ajibu kuhusu kumiliki Wasafi FM

403
0
Share:
Share this
  • 750
    Shares

Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema kuwa yeye anamilikia kwa namna moja ama nyingine anamiliki redio zote zinazohusiana na burudani na vijana nchini, na kwamba lengo la kufanya hivyo ni kutanua wigo wa muziki wa Tanzania ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi.

Kusaga ameyasema hayo leo Disemba 4, 2018 wakati akizungumza katika mahojiano mubashara kwenye kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds FM baada ya kuulizwa swali na mtangazaji mmoja.

Akifanya mahojiano hayo, mtangzaji huyo alimuuliza kama ni kweli anamiliki Wasafi FM kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na watu mbalimbali, lakini yeye akajibu na kwa kusema kuwa, hataki kwenda kwa kina kwenye hilo, lakini ukweli ni kuwa anamilikia redio zote za vijana nchini.

“Hapana, mimi sitakwenda huko. Mimi namiliki redio zote za vijana kwa njia moja ama nyingine,’ alisema Kusaga.

Aliongeza kwamba yupo pia katika redio nyingine za burudani kama vile Safari pamoja na Jembe ni Jembe FM.

Tangu kuanzishwa kwa Wasafi FM, watu wengi wamekuwa wakidai kuwa bosi huyo wa ngazi ya Clouds ndiye anamiliki redio hiyo.

Hivi karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA ilitoa ripoti ambayo ilionesha wamiliki wa Wasafi TV ambapo mmoja wa wamilikia hao ni Juhayna Zaghalulu Ajmy anayemiliki 53% ikiwa ndiye mwenye hisa nyingi zaidi.

Juhayna inadaiwa kuwa ni mzazi mwenza wa Joseph Kusaga, ambapo wengi wameona kuwa Kusaga alimtumia yeye katika umiliki wa kituo hicho cha runinga nchini.

 

Comments

error: Content is protected !!