Boti yazama Ziwa Victoria na kuua watu 29

330
0
Share:
Share this
  • 1K
    Shares

Kampala: Watu 29 wamefariki dunia, huku wengine 40 wakiokolewa na wengi wakihofiwa kuwa wamezama katika Ziwa Victoria upande wa Uganda baada ya bodi waliyokuwa wamepanda kuzama jana Novemba 24.

Boti hiyo iliyokuwa imebeba watu zaidi ya 80, ilizama jana kutokana na hali mbaya ya hewa, Jeshi la Polisi nchini humo limethibitisha.

Kamanda wa Polisi Patrick Onyango, amesema kuwa boti hiyo ilikuwa imebeba watu wengi kuliko uwezo wake, na pia kulikuwa na hali mbaya ya hewa, na kuwa ndiyo chanzo cha boti hiyo kuzama. Ameongeza kuwa, wanaendelea na zoezi la uokoaji, kuona kama wataweza kuokoa walioko hai.

Boti hiyo iliyokuwa na watu waliokuwa wanakwenda kwenye sherehe ilizama eneo la Mutima katika Wilaya ya Mukono karibu na Mji Mkuu wa Uganda, Kampala.

Ajali hiyo iliyogharimu maisha ya watu wengi ni ya pili kutoka katika ziwa hilo kwa siku za hivi karibuni, ambapo Septemba 20, 2018, watu 238 walipoteza maisha huku 41 wakiokolewa nchini Tanzania baada ya kivuko cha Mv Nyerere kupinduka katika ziwa hilo kwenye kisiwa cha Ukara wilaya ya Ukerewe jijini Mwanza.

Comments

error: Content is protected !!