Breaking: Rais Magufuli ateua Jaji Mkuu wa Tanzania

3656
0
Share:
Share this
  • 2K
    Shares
CMTL Group

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Septemba, 2017 amemteua Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Uteuzi huu unaanza leo tarehe 10 Septemba, 2017.

Kabla ya uteuzi huo Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amechukua nafasi ya Mhe. Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.

Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ataapishwa kesho tarehe 11 Septemba, 2017 saa 4:00 Asubuhi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

10 Septemba, 2017

Comments

error: Content is protected !!