Cameroon yaondolewa kuwa mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Africa (AFCON)

310
0
Share:
Share this
  • 234
    Shares

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeamua kuwa, fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 zilizopangwa kufanyika nchini Cameroon, hazitofanyika tena nchini humo kutokana na sababu za kiusalama.

CAF imefikia uamuzi huo katika kikao chake kilichofanyika kujadili hali ya kiusalama nchini Cameroon kuelekea mashindano hayo. CAF imefikia uamuzi wa kuiengua nchi hiyo kuhodhi mashindano hayo makubwa Afrika kufuatia kuwepo kwa mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa kundi la kigaidi la Boko Haram na mgogoro baina ya Jeshi na makundi ya wananchi waliojitenga katika maeneo tofauti nchini humo.

Kufuatia uamuzi huo, CAF imetoa fursa kwa nchi nyingine kutuma maombi ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo ambazo imepangwa kufanyika mwezi Juni na Julai mwaka 2019.

Katika taarifa yake, CAF imebainisha kuwa, nchi mwenyeji mpya wa michuano hiyo itatangazwa Disemba 31 mwaka huu.

Comments

error: Content is protected !!