Hii hapa tarehe na eneo la kufungia ndoa ya AliKiba

639
0
Share:
Share this
  • 432
    Shares
CMTL Group

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete ametoa nasaha zake kwa Mwanamuziki Ali Saleh Kiba maarufu Alikiba baada ya kumtaarifu kuwa anatarajia kuoa hivi karibuni.

Taarifa za kuoa kwa Alikiba zilifahamika kufuatia taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wa Twitter wa Rais Dkt Kikwete akimshukuru Alikiba kwa kumtembelea na kusema kuwa, alipata nafasi ya kumpa nasaha zitakazomsaidia katika maisha yake ya ndoa baada ya msanii huyo kumwambia kwamba ataoa hivi karibuni.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Alikiba hakuandika chochote kuhusu yeye kuoa lakini alimshukuru Rais Dkt Kikwete pamoja na familia yake kwa kupata wasaa wa kuonana nae huku amkimtakia baraka kutoka kwa Mungu.

Licha ya kuwa Alikiba hakuzungumzia suala la ndoa yake, lakini taarifa za kuaminika zimeeleza kuwa anatarajia kufunga ndoa tarehe 19 Aprili mwaka huu mjini Mombasa.

Alikiba atafunga ndoa na mpenzi wake,  Amina Khaleef ambapo imeelezwa kwamba ndoa hiyo inaandaliwa na marafiki zake wa karibu akiwamo Gavana wa Mombasa, Sultan John.

Haikufahamika mara moja kama lengo la Alikiba kwenye kwa Rais Dkt Kikwete lilikuwa kumualika ili aweze kuhudhuria ndoa hiyo ama la.

Kwa upande wake mwanamuziki Ommy Dimpoz ambaye aliambata na Alikiba amesema, ulikuwa ni wakati wa furaha walipotelea familia hiyo ya Rais Mstaafu na kupataa wasaa wa kuzungumza na kubadilishana mawili matatu.


Wasanii wamekuwa wakimpongeza Rais Dkt Kikwete na kusema kuwa, wakati wa uongozi wake wa miaka 10, sanaa ya Tanzania ilipata nafasi kubwa ya kukua na hata wasanii kwa kiasi kikubwa kunufaika na kazi zao pamoja na kutambuliwa.

Rais Dkt Kikwete mara kadhaa amekuwa akihudhuria hafla zinazohusu wasanii ambapo Aprili 2 mwaka huu alikuwa katika hafla ya utoaji tuzo za filamu za Tanzania (Sinema Zetu International Film Festival) iliyofanyika katika ukumbi eneo la Mlimani City.

Tuzo hizo ziliandaliwa na Kituo cha Runinga cha Azam ambapo zilihusisha utoaji tuzo kwa wasanii mbalimbali wa filamu za Tanzania waliofanya vizuri.

 

Comments

error: Content is protected !!