HIVIPUNDE: Familia ya Dewji yatangaza kutoa TZS bilioni 1 kwa atakayetoa taarifa alipo Mo Dewji

269
0
Share:
Share this
  • 452
    Shares

Familia ya Dewji imetangaza kutoa kiasi cha TZS bilioni moja kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa mtoto wao, Mohammed (Mo) Dewji.

Hayo yamesemwa leo na mwanafamilia mmoja wakati familia hiyo ikizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kutekwa kwa Mo Dewji.

Familia imeeleza kuwa, kwa yeyote atakayetoa taarifa hizo, taarifa atakazozitoa pamoja na utambulisho wake, vitabaki kuwa siri kati ya mtoa taarifa na familia.

Aidha, akizungumza na vyombo vya habari katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Kampuni ya MeTL Group zilizopo katika jengo la Golden Jubilee Towers, ghorofa ya 20, Mtaa wa Ohio, Posta jijini Dar es Salaam, mwanafamilia huyo amelishukuru Jeshi la Polisi kwa jitihada za kuendelea kumtafuta mtoto wao.

Pia, amewashukuru watanzania wote na watu mbalimbali ambao wamekuwa wakiendelea na maombi, huku  wakiamini kwamba mfanyabiashara huyo atapatikana akiwa salama.

Comments

error: Content is protected !!