HIVIPUNDE: Mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘atekwa’ na watu wasiojulikana

499
0
Share:
Share this
  • 779
    Shares

Taarifa zilizotufikia muda mfupi uliopita ni kuwa, mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji maarufu Mo ametekwa na watu wasiojulikana mapema leo asubuhi wakati akienda kufanya mazoezi (gym) eneo la Colosseum jijini Dar es Salaam.

Wafanyabiashara wengi na viongozi mbalimbali hupendea kufanya mazoezi eneo hilo (Colosseum Gym).

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa, watu hao walifyatua risasi angani wakati Mo akiingia gym na kisha kuondoka naye.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Jeshi la Polisi linafuatilia taarifa za madai ya kutekwa kwa mfanyabiashara, Mohammed Dewji leo asubuhi.

Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zitakujia.

Comments

error: Content is protected !!