Idadi ya watu waliouawa kutokana na vurugu za uchaguzi Kenya

807
0
Share:
Share this
CMTL Group

Tume ya Haki za Binadamu nchini Kenya (KNCHR) imesema kuwa watu 24 wameuawa tangu kuanza kwa kipindi cha uchaguzi tangu Agosti 8.

Katika taarifa iliyotolewa na tume hiyo imeeleza kuwa watu 17 wameuawa katika mji wa Nairobi City, Homabay wameuawa 2, Kisumu ameuawa 1, Migori 2 na Siaya wameuawa watu 2.

Wakielezea chanzo cha mauaji hayo, tume hiyo ilisema wengi wameuawa kwa kufyatuliwa risasi wakati wakiandamana katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Taarifa hiyo imekuja wakati chama cha upinzani kimesema kuwa zaidi ya watu 100 wameuawa lakini hawakutoa uthibitisho wowote wa madai hayo.

Hapa chini ni taarifa ya tume hiyo kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu;

Comments

error: Content is protected !!