Ifahamu vyema ndege mpya ya Tanzania Boeing 787-8 Dreamliner inayotua leo

1053
0
Share:
Share this
  • 1.2K
    Shares
CMTL Group

                              Ikiwa katika uwanja wa ndege wa Paine Seattle Marekani tayari kwa safari

Ndege ya Boeing 787-7 Dreamliner ni mojawapo ya ndege toleo la Boeing 787 ambazo zinatengezwa na kampuni ya Boeing Commercial Airplanes ya nchini Marekani ikiwa ni moja ya makampuni makubwa kabisa ya uundaji wa ndege. Ndege hizi zimeundwa kwa safari ndefu na zina engine mbili. Ndege za toleo la 787 pia zimeundwa kuwa na ubora wa asilimia 20 zaidi katika matumizi ya mafuta, tofauti na toleo la awali la 767.

Eneo la rubani

Awali waundaji wa ndege hizi walitaka kuzipa jina la 7E7 lakini mwezi Januari 2005 walibadilisha. Ndege ya kwanza katika mlolongo wa 787 ilizinduliwa rasmi Julai 8 2007 huko Everret Washington na kisha kuingia sokoni takribani mwaka mmoja baadaye, Mei 2008. Safari ya kwanza kabisa ya ndege hiss ilikuwa Disemba 15, 2009. Inaripotiwa kuwa kampuni ya Boeing imetumia shilingi za Kitanzania zaidi ya trilioni 65 katika biashara yake ya kuunda ndege hizi za mfumo wa 787. Matoleo yaliyoundwa mpaka sasa ni 787-8, 787-9 na 787-10.

  Daraja la Tatu (Economy Class)

787-8 ambayo ndiyo iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania na inatarajiwa kutua leo Jijini Dar Es Salaam kawaida ina uwezo wa kubeba abiria 242 na ziliingia sokoni mwaka 2011 kuchukua nafasi ya Boeing 767-200ER na -300ER. Ndege hizi za 787-8 zinaonekana kuwa bora katika matumizi ya mafuta na masafa marefu. Karibu asilimia 32 ya oda za matoleo ya 787 ni za 787-8 na hadi kufikia Mei 2018 ndege 351 zilikuwa tayari zimenunuliwa na wateja mbalimbali duniani. Baadaye mwaka huu, Boeing itaanza uzalishaji wa 787-9 na 787-10 kuboresha zaidi soko lake.

                                         Business Class

Kiwanda cha Boeing Everett Washington Marekani

 

Mhandisi William Boeing mwanzilishi wa kampuni ya Boeing

Comments

error: Content is protected !!