IGP Sirro awashukia Askari wanaokimbilia kutoza faini

853
0
Share:
Share this
  • 2.9K
    Shares
CMTL Group

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, (IGP) Simon Sirro amewataka Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutokutoza faini mara zote mtu anapovunja sheria, bali wakati mwingine watumie busara kutoa elimu pamoja na onyo kabla ya kuamua kutoza faini.

IGP Sirro amesema si busara kumtoza dereva faini mara moja anapokosea bali unaweza ukampa elimu kuwa jambo analolifanya si sahihi na huenda likahatarisga usalama wake au wa watumiaji wengine wa barabara, au akapewa onyo ili atakaporudia tena kosa hilo, atozwe faini.

“Jambo la kwanza la kuzuia uhalifu ni elimu, siku ya pili onyo na siku ya tatu ni faini, sio unaanza kwa faini pasipo kumpa elimu wala onyo.”

Kiongozi huyo wa Polisi aliyasema hayo jana alipokuwa ziarani mkoani Iringa, Sirro na kukanusha madai yanayotolewa kwenye mitandao ya kijamii kwamba polisi wamepangiwa kiwango cha faini cha kukusanya kwa siku.

Sirro alisema wakati mwingine Polisi hao hutoka makwao wakiwa na makwazo mabalimbali na hivyo kuhamishia hasira kwa madereva wanaovunja sheria barabarani, hivyo akawasihi wananchi wawavumilie kwani nao ni wanadamu.

Comments

error: Content is protected !!