Kauli ya mwisho ya CCM ‘mvutano’ wa Katibu Mkuu, Dkt Bashiru na Bernard Membe

308
0
Share:
Share this
  • 520
    Shares

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeingilia kati mvutano unaoendelea kati ya Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally na mwanachama wa chama hicho Bernard Membe na kusema kwamba, mijadala inayohusu kauli ya katibu huyo imepotoshwa na kwamba haina tija.

Kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, chama hicho kimeeleza kuwa kimesikitishwa na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii kuhusu wito wa kiongozi wa chama hicho kutaka kuonana na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe.

“CCM inapenda kuwafahamisha kuwa imefuatilia kwa ukaribu mjadala unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wito alioutoa Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM kwa Ndg. Benard Membe ambaye ni Mwanachama wa CCM kama sehemu ya utaratibu wa kawaida wa Katibu Mkuu kukutana na Viongozi na Wanachama wa CCM katika kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa wanaCCM” alisema Polepole.

Chama hicho kimetoa rai kwa watanzania kuwa wito wa Katibu Mkuu ulikuwa ni wito wa kawaida wa kiongozi wa CCM kwa mwanachama wa CCM, hivyo uzushi, uchonganishi, fitina na uvumi mwingine wowote unaoendelea hasa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya magazeti yenye hila mbaya, wana CCM na umma wa watanzania wanaombwa waupuuze.

Dkt Bashiru akiwa katika moja ya mikutano ya ndani ya chama hicho alimtaka Bernard Membe kufika ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo kufuatia kuwepo kwa tetesi kupitia baadhi ya magazeti na mitandao ya kijamii kuwa, mwanachama huyo alikuwa akifanya kampeni za chini chini ili kugombea urais mwaka 2020.

Comments

error: Content is protected !!