Kauli ya serikali kuhusu ulaji wa nyama ya kuku wa kisasa

669
0
Share:
Share this
  • 1K
    Shares

Serikali imesema kuku wa kisasa ambao hutumiwa kwa ajili ya kitoweo/nyama (Broilers) hawana madhara kiafya kwa binadamu kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakisema.

Hayo yamesemwa leo Novemba 16, 2018 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati akijibu swali la mmoja wa wabunge lililoelekezwa katika wizara hiyo.

Naibu Waziri Ulega amesema kuwa, dawa na vyakula ambavyo vinatumika kwa kuku hao kwa ajili ya kuwakuza vimekuwa vikifanyiwa utafiti, na vimebainika kuwa na ubora unaostahili.

Baadhi ya wabunge walionesha hofu yao kuhusiana dawa na vyakula wanavyokula kuku hao, kuwa vimekuwa vikileta mabadiliko hasi kwa baadhi ya walaji wake.

Mbali na bungeni, ndani ya jamii kumekuwa na maoni tofauti tofauti kutoka kwa wananchi kuhusu ulaji wa kuku hao, huku wengi wakiamini wana madhara kiafya, na hivyo kupelekea kupunguza ulaji, kuacha kabisa au kutumia kuku wa kienyeji.

Comments

error: Content is protected !!